Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi, amefariki dunia.

Kifo cha Lukuvi kimechotokea leo Machi 25, 2026, majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia mshtuko wa moyo.
Taarifa ya msiba huo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na kuthibitishwa kwa kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka.
Kufuatia kifo cha Waziri Lukuvi, rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, ameeleza masikitiko yake kuhusu kifo hicho.
" Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya kifo cha Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Ismani.Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa kwa Taifa, uongozi wake thabiti na uzalendo wake uliotukuka katika kulitumikia Taifa kwa muda mrefu.Ninatoa pole za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa msiba huu mzito"
Hayati Lukuvi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akisimamia sera, uratibu wa shughuli za Serikali pamoja na masuala ya watu wenye ulemavu.

No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.