WALIODAI KUPOTEZA KIMIUJIZA SEHEMU ZAO ZA SIRI SHINYANGA WASHIKILIWA NA POLISI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wawili wakazi wa Wilaya ya Kahama, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo na kuzua taharuki kwa madai ya kupoteza kimiujiza sehemu zao za siri.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amesema tukio la kwanza limetokea
Aprili 4, 2026 katika eneo la soko kuu mjini Kahama, ambapo Kisaka
Elinihaki (22) alidai kupoteza sehemu zake za siri baada ya kushikwa bega la kushoto
na Joseph Godfrey (36).
Tukio hilo
lilisababisha wananchi kujaribu kumshambulia Godfrey kabla ya kuokolewa na
polisi.
Amesema
tukio la pili lilitokea Aprili 6, 2026 katika eneo la machimbo ya dhahabu
Mwime, Kahama, ambapo Makoye James alitoa madai kama hayo dhidi ya Hamis
Kumalija ambaye walikuwa wakisafiri naye kwenye Pikipiki, hali iliyosababisha
mkusanyiko wa wananchi waliotaka kujichukulia sheria mkononi, kabla ya
kudhibitiwa na Polisi.
Kamanda
Magomi amesema uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa madai ya watu hao si ya
kweli, kwani hawakuwa na mapungufu yoyote kwenye sehemu zao siri.
Amesema
watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa kutoa taarifa za uongo na kusababisha
taharuki, na hatua za kisheria zinaendelea.
Aidha,
ametoa wito kwa wananchi kuacha kusambaza taarifa za uongo na badala yake washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudumisha amani.
Post a Comment