NAFASI KUBWA YA MWANAMKE KWENYE JAMII, SABABU YA KULAUMIWA KILA MAMBO YANAPOHARIBIKA

 

Wanawake wameaswa kutambua nafasi kubwa waliyonayo ndani ya jamii pamoja na kuwajibika ipasavyo ili kuepuka kulaumiwa pale mambo yanapoharibika.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwinjilisti Salome Stephene kutoka Kanisa la AICT Ndembezi, katika Manispaa ya Shinyanga, wakati akiwahubiria mamia ya wanawake kutoka makanisa yanayounda Umoja wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Kanda ya Ndembezi.

Mwinjilisti Salome Stephene

Mahubiri hayo yametolewa katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maombi Duniani kwa Wanawake wa CCT, yaliyofanyika kikanda katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kaanani, Ndembezi mjini Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Katika ujumbe wake, Mwinjilisti Salome amewataka wanawake kutokukata tamaa wanapolaumiwa pale mambo yanapoharibika ndani ya  familia na jamii, na badala yake wanapaswa kuhakikisha wanawajibika ipasavyo ili kukidhi matarajio ya jamii ambayo inawategemea kwa mambo mengi ikilinganishwa na wanaume.

Aidha, amewasihi wanawake kuwa na subira wanapokumbana na changamoto mbalimbali katika maisha, badala ya kuwakimbilia watu wasiofaa, wakiwemo baadhi ya wanaojiita manabii ilhali wanatumikia nguvu za giza.

Amesema kabla ya kuwafuata watu hao kwa ajili ya msaada wa kiroho, ni muhimu kwanza kuwapima kwa kuzingatia Neno la Mungu ili kuepuka kupotoshwa.

Vilevile, Mwinjilisti Salome ametumia fursa hiyo kuwaasa wanawake wa Kikristo kuendelea kumtegemea Mungu pekee na kuacha kuchanganya imani ya Kikristo na ushirikina, akibainisha kuwa tabia hiyo mara nyingi huchangia kuchelewesha majibu ya maombi yao.

Katika maadhimisho hayo, wanawake walifanya maandamano kabla ya ibada maalum ya maombi, ambapo waliombea familia, ndoa pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na kuwazuia kutimiza wajibu wao ipasavyo ndani ya familia na jamii.

Wanawake wa CCT Kanda ya Ndembezi wakiwa kwenye maandamano


Wanawake wa CCT Ndembezi wakiwa kwenye maandamano kuelekea Kwenye Kanisa la KKT Usharika wa Kaanani Ndembezi



Maandamano yakiingia kwenye eneo la Kanisa la KKKT Kaanani Ndembezi

Wachungaji na wainjilisti kutoka Makanisa mbalimbali yanayounda CCT Kanda ya Ndembezi wakipokea maandamano

Wachungaji wakiomba baada ya kupokea maandamano


Makamu Mwenyekiti wa Iadara ya wanawake CCT Kanda ya Ndembezi Winifrida Kalubae akitoa utaratibu wa Ibada

Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomoni Nalinga Najulwa akiwa kwenye Ibada

Joyce Yusuph Tambe akisoma Risala ya wanawake wa CCT kwa Mgeni rasmi

Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake ya CCT Kanda ya Ndembezi Vumilia Swebe akiwatambulisha viongozi kutoka Makanisa yanayounda CCT Kanda ya Ndembezi

Mchungaji John Lyanga kutoka Kanisa kuu la KKKT Ebeneza mjini Shinyanga ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi akimpongeza Mwenyekiti wa Idara ya wanawake CCT wa Kanda ya Ndembezi           

Mchungaji John Lyanga kutoka Kanisa kuu la KKKT Ebeneza mjini Shinyanga ambaye alikuwa ni Mgeni rasm akizungumza na wanawake kabla ya kuongoza Harambee maalum kwa ajili ya wenye uhitaji


Baadhi ya viongozi wa Idara ya Wanawake kutoka Makanisa mbalimbali yanayounda umoja wa CCT Kanda ya Ndembezi
















No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.