POLISI SHINYANGA KUCHUNGUZA MADAI YA MAFUTA KUCHANGANYWA NA MAJI

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), linaendelea kuchunguza madai ya kuwepo kwa mafuta yaliyochanganywa na maji katika kituo kimoja cha mafuta mjini Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amesema uchunguzi huo unafanyika kufuatia malalamiko ya wamiliki wanne wa magari waliodai magari yao kupoteza nguvu baada ya kujaza mafuta katika kituo hicho.

Amesema walalamikaji wanahisi mafuta waliyonunua huenda yalichanganywa na maji, hivyo uchunguzi wa pamoja na wataalamu wa EWURA unaendelea ili kubaini ukweli wa suala hilo.

Kamanda Magomi amewataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea, akisisitiza kuwa majibu sahihi ya kisayansi yatatolewa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kitaalamu.

 

No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.