CP HAMDUNI AZINDUA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni, amezindua rasmi kimkoa zoezi la chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 10, linalofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jumanne, Machi 24, 2026 hadi Ijumaa, Machi 27, 2026.

Hamduni ambaye alikuwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa kwenye uzinduzi huo, amewahimiza wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo hiyo ya matone, inayolenga kuwakinga dhidi ya ugonjwa hatari wa Polio.

Aidha, ametoa onyo kwa watu watakaojaribu kupotosha umma kuhusu chanjo hiyo, akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Tina Atinda, amesema chanjo hiyo inatolewa katika mikoa saba inayopakana na Mkoa wa Mwanza, ikiwa ni hatua ya tahadhari ya kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo na kuzuia ulemavu wa ghafla.

Ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na kubainika kwa vimelea vya Polio katika majitaka yaliyopimwa hivi karibuni mkoani Mwanza.

Uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika katika Shule ya Msingi Mapinduzi (B), iliyopo Manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Tina Atinda, Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Bi. Anne Shuma, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, pamoja na Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Salum Kitumbo.

Wengine ni Diwani wa Viti Maalum Kata ya Ngokolo, Veronica Masawe, pamoja na wazazi, walezi na watoto.

Jumla ya watoto 781,186 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo katika Mkoa mzima wa Shinyanga.

Chanjo itatolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya, shuleni pamoja na kupitia mkakati wa nyumba kwa nyumba.

CP Hamduni akijiandaa kumachanja mmoja wa wanafunzi waliohudhuria zoezi la uzinduzi

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Tina Atinda akizungumza kwenye uzinduzi

Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa zoezi la chanjo

CP Hamduni akizindua zoezi la chanjo kwa kuwachanja baadhi ya wanafunzi waliohudhuria uzinduzi

CP Hamduni akiwawekea alama wanafaunzi aliowachanja

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo akizungumza kwenye uzinduzi wa chanjo

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Said kitinga akimkaribisha Mgeni rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa chanjo

CP Hamduni akinawa mikono kwa ajili ya kwenda kuzindua zoezi la chanjo

CP Hamduni akielekea kwa wahudumu wa afya kwa ajili ya kuzindua zoezi la chanjo

CP Hamduni akizungumza na Mwakilishi kutoka TAMISEMI

 

No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.