SHUWASA KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA USAMBAZAJI WA MAJI



Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeahidi kuendelea kuboresha huduma za usambazaji wa maji, ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto ndogondogo zinazojitokeza.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kupitia kikao kazi kilichofanyika leo tarehe 14, Machi, 2026, Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola, ameeleza hatua ambazo mamlaka hiyo inazichukua ili kuboresha huduma za usambazaji wa maji, ambazo ni pamoja kuimarisha miundombinu na kupanua mtandao wa maji kuyafikia maeneo ambayo yalikuwa bado hayajafikiwa na huduma hiyo.


Katopola pia aliwaomba waandishi wa Habari kuendelea kuwahabarisha wananchi juu ya namna ambavyo SHUWASA inafanya juhudi kuhakikisha wanapata huduma za uhakika za maji, ili wawe na ufahamu wa kutosha kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo.

Ameahidi kuwa, SHUWASA itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu huduma za maji, miradi inayoendelea pamoja na changamoto zinazojitokeza katika sekta hiyo.

Kwa upande wao, waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho, wameshauri mambo kadhaa ili kuifanya SHUWASA kuwa bora zaidi katika utoaji wa huduma na wameahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo kwa kuandika Habari ambazo zitaongeza uelewa kwa wananchi, kwa kuwa suala la maji linagusa hitaji muhimu la watu.

No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.