Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kaanani, Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa ziwa Victoria, Winston Kweka, amewaasa Wakristo kuwajali na kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Mchungaji Kweka ametoa ujumbe huo katika Ibada maalum ya matendo ya huruma, ambayo imewashirikisha wanawake kutoka makanisa yanayounda Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) tawi la Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga, iliyofanyika kwenye Kanisa la Usharika wa Kaanani Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi mjini Shinyanga.
Amewaasa Wakristo wote kuwa na huruma kwa watu wenye uhitaji, na kuwasaidia kadiri ya mahitaji yao, wakifuata mafundisho na mfano wa Bwana wao Yesu Kristo, aliyejitoa kwa ajili ya wengine.
Mchungaji Kweka amewataka wakristo kutokubali kumuona mtu mwingine akiishi maisha ya shida huku wao wakiishi vizuri na kwamba, wanapotoa msaada kwa wenye uhitaji wasibague kwa misingi ya kabila, wala imani yao.
Mchungaji huyo amebainisha kuwa, kufanya matendo ya huruma ni nafasi nzuri ya kumtukuza Mwenyezi Mungu na kuendelea kupokea baraka zake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake ya CCT tawi la Ndembezi Bi.Vumilia Swebe, amewaomba wanawake wenzake kuendelea kuguswa na hali ya watu wenye uhitaji, kwa kuwa bado kuna kundi kubwa kwenye jamii ambalo linahitaji msaada kutoka kwa wengine.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Bw. Solomoni Nalinga Najulwa, aliwapongeza wanawake wa CCT tawi la Ndembezi kwa kushirikiana na Kanisa la KKKT kuona umuhimu wa kuwajali wenye uhitaji, hatua ambayo ameitaja kuwa ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na Wakristo wengine, hasa katika kipindi hiki cha Kwaresima, ambacho kinahimiza waumini kuonyesha upendo na kujitoa kwa ajili ya wengine.
Wanawake hao wa CCT tawi la Ndembezi wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watu wenye uhitaji ikiwemo mavazi na sabuni, ambavyo wamevikusanya kama majitoleo yao, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maombi ya wanawake duniani, ambayo kilele chake ni kesho Ijumaa tarehe, 06,2026.
Kilele cha siku ya maombi ya wanawake wa CCT, katika tawi la Ndembezi kitafanyika kwa Ibada maalum itakayofanyika kwenye Kanisa la KKKT usharika wa Kaanani, Ndembezi.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA IBADA YA MATENDO YA HURUMA KWA WANAWAKE WA CCT TAWI LA NDEMBEZI ILIYOONGOZWA NA
Wanawake wakiwa kwenye Ibada ya Matendo ya Huruma

Ibaada inaanza
Mchungaji Kweka wa Kanisa la Kaanani akiongoza Ibada
Ibada inaendelea
Mchungaji Kweka akiendelea na Ibada



Ibada inaendelea
Mchungaji Kweka akifuatilia Neno la Mungu wakati wa somo
Mwenyekiti wa CCT tawi la Ndembezi Vumilia Swebe akisoma Neno la Mungu
Ibada inaendelea
Mchungaji Kweka akitoa tafakari ya Neno la Mungu

Ibada inaendelea

Viongozi wa CCT tawi la Ndembezi wakiandaa vitu mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya msaada
Mchungaji Kweka akiongoza sala kubariki Misaada ya watu wenye uhitaji

Viongozi wa CCT Ndembezi wakigawa misaada kwa wenye uhitaji
Mwenyekiti wa Idara ya wanawake CCT tawi la Ndembezi Vumilia Swebe akitoa maelekezo
Hatua mbalimbali za kuwasaidia wenye uhitaji zinaendelea
Baadhi ya wazee walioshiriki Ibada hiyo

Mwenyekiti wa Idara ya wanawake CCT Ndembezi akizungumza mara baada ya zoezi la kugawa misaada
Hatua mbalimbali zinaendelea
Mchungaji Kweka akitoa neno la Shukrani
Wanawake wa CCT wakiwa nje ya Kanisa baada ya Ibada
Picha mbalimbali za nje ya Kanisa za wanawake wa CCT, Mchungaji Kweka na Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Solomoni Nalinga Najulwa (Mwenye Skafu ya Bendera ya taifa)

Bw. Najulwa akisalimiana na Mchungaji Kweka
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Solomoni Nalinga Najulwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Idara ya Mwanawake KKKT Ndembezi Winifrida Kalubae
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome akisalimiana na makundi mbalimbali ya Wanawake
Bw. Najulwa akizungumza na akina Mama wa CCT Ndembezi
Post a Comment