MWILI WA KARDINALI PENGO WAPOKELEWA KATIKA KANISA KUU LA MT.YOSEFU


Mwili wa Hayati Mwadhama  Polycarp Kardinali Pengo umepokekewa katika KanisaKuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kutoka katika Hospitali ya Lugalo.

Mwili umewasili asubuhi majira ya saa tatu kasorobo na Kupokelewa na Mhashamu Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Msaidizi Henry Mchamungu, Abate, Mapadre, Watawa na Waaamini mbalimbali.

Baada ya Mapokezi Askofu Mkuu Aliongoza Sala Fupi ya Kumwombea na kuweka Alama za Kichungaji Juu ya jeneza lake na kuandamana hadi Kanisanni ambapo Waamini na watu mbalimbali wanaendelea na Utaratibu wa Kutoa Heshima za Mwisho pamoja na kushiriki Misa za kumwombea, ambazo zitafuatiwa na mkesha wa Sala na maombolezo.

Mazishi ya Kardinali PENGO yatafanyika kesho katika kituo Cha hija Pugu,na yatatanguliwa na Misa takatifu ya kumwombea ambayo inatarajiwa kuanza saa 4:00 asubuhi.

Mungu ampe Pumziko la Milele Hayati Kardinali Pego, AMINA.


CHINI NI PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI BAADA YA MWILI KUPOKELEWA KATIKA KANISA KUU LA MT. YOSEFU



















(Picha na Jugo Media)



No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.