KATAMBI AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA YA NGUZONANE MWAWAZA KUACHA VISINGIZIO VINAVYOCHELEWESHA MRADI



Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Paschal Patrobas Katambi, ameiagiza kampuni inayojenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Ngunzonane kuelekea Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga (Mwawaza) kurekebisha mara moja kasoro zinazochelewesha utekelezaji wa mradi huo.


Katambi ametoa agizo hilo Jumatatu, Februari 23, 2026, baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kusuasua kwa mradi.


Katika ziara hiyo, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuacha visingizio na kuhakikisha anaondoa kasoro zote zinazokwamisha utekelezaji kwa kuzingatia masharti ya mkataba.


Amesisitiza kuwa endapo hali hiyo itaendelea, yeye kama Mbunge hatasita kuchukua hatua zaidi kulingana na taratibu za kisheria.


Mbali na mradi huo wa barabara, Katambi pia alikagua ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi kinachojengwa katika eneo la Katunda, mradi ambao pia unatekelezwa na kampuni hiyo.


Miradi yote miwili kwa pamoja ambayo inatekelezwa na Kampuni ya SIHOTECH ENGINEERING COMPANY AND AMJ GLOBAL MULTI COMPANY LIMITED JV ya Jijini Dodoma, itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 26 mpaka kukamilika kwakwe.


Miradi hiyo ambayo utekelezaji wake ulianza mnamo tarehe 21, Julai, 2025, inatarajiwa kukamilika tarehe 18, Oktoba, 2026.

Hatua ya ujenzi wa Barabara ilipo

Katambi akizungumza na Viongozi wa Kampuni inayojenga Barabara








Wananchi wakiwa kwenye eneo la barabara inayojengwa wakifuatilia maelekezo ya Mbunge wao.

Sehemu tofautitofauti ya Barabara inayojengwa





Mwonekano wa baadhi ya sehemu za Barabara inayojengwa




No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.