UJENZI WA DARAJA LA DODOMA MAKABURINI MJINI SHINYANGA KUKAMILIKA MAPEMA MWEZI UJAO

Mradi wa ujenzi wa daraja la Gagi road linalojengwa katika eneo la Dodoma Makaburini mjini Shinyanga, unatarajiwa kukamilika katikati ya mwezi ujao tarehe 15 Machi, 2026.


Kwa mujibu wa Meneja wa Wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) wa Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Pamphili, daraja hilo linalounganisha mitaa ya Mageuzi (Kata ya Ngokolo) na Butengwa (Kata ya Ndembezi) linatarajiwa kuanza kutumika mara baada ya kuzinduliwa.


Meneja huyo wa TARURA, ameeleza kuridhishwa na hatua za ujenzi wa daraja hilo, mradi ambao umeanza kutekelezwa tarehe 15, Desemba, 2026, na Kampuni ya Sabu Enteprises Co. Limited ya mkoani Shinyanga chini ya usimamizi wa Kampuni ya Norplan Tanzania Limited ya Jijini Dare es salaam.


Mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 105 mpaka kukamilika kwake.
Daraja hilo, lililotajwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Paschal Patrobas Katambi, kuwa ni miongoni mwa mafanikio yaliyowagusa moja kwa moja wananchi wa Shinyanga katika siku 100 za uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, linatarajiwa kuondoa changamoto ya muda mrefu iliyokuwa ikiwasumbua wananchi wa Kata za Ngokolo na Ndembezi. 


Wananchi hao wanategemea barabara zinazounganishwa na daraja hilo, ambalo hapo awali lilikuwa kikwazo kikubwa cha usafiri na kuhatarisha maisha yao, hususan katika kipindi cha mvua. 

Redio Faraja imeshuhudia ujenzi wa daraja hilo, ukiendelea.
 

  CHINI NI PICHA MBALIMBALI ZA MWO NEKANO WA HATUA ZA UJENZI WA DARAJA





























No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.