ASKOFU MWOMBEKI AWAONGOZA WAKAZI WA SHINYANGA KATIKA MKESHA WA KINABII-WATU WATOA SHUHUDA MBALIMBALI
Askofu Edsoni Mwombeki wa Kanisa la Emmanuel, lililopo Ngokolo mjini Shinyanga, amewaongoza wakazi wa Shinyanga, wakiwemo washirika wa kanisa hilo, katika mkesha maalum wa kinabii uliolenga kumshukuru Mungu na kufanya maombi kwa ajili ya nia mbalimbali.
Mkesha huo umefanyika usiku wa kuamkia Jumapili, Machi 1, 2026, katika Ukumbi wa Makindo uliopo mjini Shinyanga ambapo watu waliohudhuria walishiriki maombi maalum, kufanya toba pamoja na kutoa ushuhuda kuhusu namna wanavyoamini kuwa Mungu amewatendea kupitia maombi waliyofanyiwa na Askofu huyo.
Akizungumza wakati wa mkesha huo, Askofu Mwombeki aliwahimiza Wakristo kwa ujumla wao kuendelea kumtegemea Mwenyezi Mungu katika maisha yao, akisisitiza kuwa, hakuna jambo lisilowezekana kwa wale wanaomwamini na kumwabudu kwa roho na kweli.
Aidha, alifanya maombi maalum kwa ajili ya makundi mbalimbali ya watu, wakiwemo wanawake, wanafunzi na watu wenye mahitaji.
Askofu Mwombeki anaendelea kutoa ushuhuda wa kinabii kuhusu ukuu wa Mungu, baada ya kutoka Gerezani alikokaa kwa takribani miaka kumi, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 Gerezani.
Baada ya kutoka Gerezani kwa msaada wa kisheria aliopewa kupitia Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Askofu Mwombeki alirudi kwenye huduma huku akibainisha kuwa, muda aliokaa Gerezani umekuwa chachu ya kumfanya aongeze nguvu zaidi ya kumtumikia Mwenyezi Mungu, pamoja na kutoa ushuhuda mara kwa mara kwa wengine juu ya nguvu, uwezo na ukuu wa Mungu.
Leo Jumapili, atawaongoza baadhi ya washirika wa Kanisa hilo pamoja na watu wenye mapenzi mema kwenda kuwaona wafungwa Gerezani na kutoa msaada, ikiwa ni ishara ya kuguswa na shida za wengine, kuonyesha moyo wa huruma na kuwajali watu wanaohitaji msaada na faraja kutoka kwa jamii.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MKESHA
Askofu Edsoni Mwombeki akiwa ameketi baada ya kuwasili ukumbini tayari kwa mkesha
Washiriki wa mkesha wakiendelea na Ibada
Baadhi wa washiriki wa Mkesha kutoka Jijini Mwanza wakitoa ushuhuda wa kiimani
Washiriki wa mkesha wakifuatilia neno la Mungu
Askofu Mwombeki akifundisha Neno la Mungu kwa washiriki wa mkesha
Washiriki wa mkesha wakishangilia Neno la Mungu
Washiriki wa mkesha wakiendelea kufuatilia Neno la Mungu
Washiriki wa Mkesha wakiimba na kusifu
Askofu Mwombeki akiwaongoza washiriki wa Mkesha katika sifa na kuabudu
Washiriki wakiendelea kusifu na kuabudu
Post a Comment