KARDINALI KAMBANDA ATOA WITO KWA WANAHABARI WAKATOLIKI KUWA KICHOCHEO CHA AMANI NA UMOJA


KIGALI-RWANDA’

Na Anatoli Salawa

Wito umetolewa kwa waandishi wa habari na wataalamu wa tasnia ya habari wa Kanisa Katoliki kutumia fursa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kujenga utamaduni unaoleta amani katika familia ya binadamu, kwa kuandaa maudhui yanayokuza umoja, mshikamano na kuheshimu utu.

 Hayo yameelezwa na Askofu Mkuu wa JImbo Kuu la Kigali nchini Rwanda, Mwadhama ANTONI Kardinali  KAMBANDA, wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Kimataifa la SIGNIS linaloendelea huko Kigali nchini Rwanda.

 Akitoa ujumbe wake katika Kongamano hilo, Kardinali Kambanda ameonya juu ya matumizi mabaya ya vyombo vya habari na kwa namna ya pekee kwa wakati huu ambapo mawasiliano ya kidijitali yamekuwa ndiyo nyenzo ya kufikisha ujumbe kwa muda mfupi kuliko wakati wowote.

 Amesema kuwa katika ulimwengu huu wa kidijitali vyombo vya Habari vinaweza kuwa nyenzo zenye nguvu na uwezo wa kubomoa na kuingiza hofu kwa jamii ya binadamu kwa haraka kama vitasimamiwa na watu wasio na nia njema ya kujenga na kuileta jamii pamoja na badala yake wakajikita katika kuboa misingi ya umoja, amani na mshikamano.

Ametolea mfano mauaji ya kutisha yaliyofanyika nchini Rwanda mnamo Mwaka 1994,kuwa yalichangiwa na chombo cha Habari ambacho kilichochea taharuki na mauaji ya kutisha ambayo yalileta machozi na maumivu kwa wanarwanda kwa miaka mingi. 

Amewaasa wanahabari wa Kanisa Katoliki kubeba wajibu mkubwa wa kuendelea kuponya majeraha hayo kwa kuandaa maudhui ya upatanisho.

 Aidha ametoa wito kwa, waandishi wa Habari na wanaosimamia vyombo vya Habari vya kanisa kuleta mabadiliko katika tasnia ya Habari wakilenga kumkomboa mwanadamu mzima kimwili na Kiroho.

 SIGNIS Ni Shirika la Kanisa Katoliki linalosimamia Vyombo vya Habari na Wanahabari katika Kanisa Katoliki Ulimwenguni. 

Zaidi ya wanahabari wa Kanisa katoliki miambili sitini kutoka nchi mbalimbali duniani wanashiriki Kongamano hilo, ambapo washiriki Zaidi ya ishirini ni wanahabari Wakatoliki kutoka Tanzania.

Baadhi ya Maaskofu wakiwa kwenye Misa ya ufunguzi wa Kongamano

Wanahabari kutoka mataifa mbalimbali wakiwa kwenye Misa ya ufunguzi wa Kongamano


Mapadre ambao wengi wao ni wataalam wa masuala ya Habari na Mawasiliono kutoka mataifa mbalimbali wakiwa kwenye  Misa ya ufunguzi wa Kongamano
Wanakwaya

Tanzania.

No comments

#tuandikie maoni yako.

Theme images by Storman. Powered by Blogger.